Monday, May 14, 2018

JE WAJUA SAA YENYE MOYO KAMA WA BINADAMU?

Ndio najua bado kichwani mwako unajiuliza saa zenye moyo wa binadamu kivipi? basi mwandishi wa makala hii ndo kazi yangu kukupa majibu na elimu kuhusu saa zenye moyo... 


Tuanzie hapa msomaji saa zenye moyo kwa lugha sahihi ya kiswahili ni saa ambazo hazitumii battery yaani kiingereza automatic watch/mechanical watches....katika ulimwengu huu wa saa basi saa hizi ndo zilikuwa za kwanza kugunduliwa saa hizi ziligunduliwa na peter henlein wa mji wa nuremberg ujerumani....wakati saa za mabattery ziligunduliwa mwaka 1955 yaani quartz watch huko japani ..... baada ya historia fupi hiyo ngoja sasa tuone uchawi wa mzungu huyu peter henlein alifanyaje saa hizi hazitumii battery tutamia lugha nyepesi kila mtu asomae makala hii aelewe na video nitaweka
 
1.SAA HIZI HUPATA NGUVU UNAPOTIKISA MKONO WAKO
chazo kikubwa cha nguvu za saa hizi huwa mtu alivaa saa hii akiwa anatembea anavyotikisa mkono basi saa hizi kama unajua wana fikia hapa wataelewa saa hii huchukua motion energy na kuifadhi nguvu hii kwenye spiringi kuu (main spring)yaani saa hii uko zako mishe mishe zako unatembea ..na yenyewe inakuwa bize inachaji jinsi unavyotisa mkono.....
 
2. INA GIA
mi ndo maana nasemaga wazungu bwana kwenye ugunduzi ni watu hatari saa hizi bwana zina mfumo wa gia ...gia hizi bwana zinafanya kazi kwa waledi wa hali ya juu yaani kubadilisha nguvu ya mtetemeko wa mkono wako na kuziifadhi kwenye spiring kuu yaaani huu sasa NDO HUITWA MOYO wa saa yaani ukizima na saa inasimama kana kwamba binadamu moyo ukizima nae anakufaaa....lakini saa hizi moyo huu wa saa ni kwamba ukitisaa tu mkono na moyo wa saa unaanza kufanya kazi ...ngoja niwekee mfano saa ya kampuni t winner ambayo nayo ni moja ya SAA AMBAYO INA MOYO

 👑SIRI YA HERUFI YA MWANZO YA JINA LAKO👑
 🌼HERUFI A
 Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.

 🌼HERUFI B
 wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.

 🌼HERUFI C
 Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano.

 🌼HERUFI D
 Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.

 🌼HERUFI E
 Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.

 🌼HERUFI F
 Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.

 🌼HERUFI G
mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.

 🌼HERUFI H
 Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.

 🌼HERUFI I
 Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.

 🌼HERUFI J
 Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.

 🌼HERUFI K
 Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha.

 🌼HERUFI L
 Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.

 🌼HERUFI M
 Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.

 🌼HERUFI N
 Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.

 🌼HERUFI O
 Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.

 🌼HERUFI P
 Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.

 🌼HERUFI Q
 Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.

 🌼HERUFI R
 Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.

 🌼HERUFI S
 Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.

 🌼HERUFI T
 Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.

 🌼HERUFI U
 Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi.

 🌼HERUFI V
 Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.

 🌼HERUFI W
 Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari.

 🌼HERUFI X
 Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.

 🌼HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha.

 🌼HERUFI Z
 Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo,
 je na jina lako lina maana gani? Jibu usione aibu!




MTOTO WA KIUME AU WA KIKE ANATOKEAJE?


MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUAMUA JINSIA
1.Lazima mwanamke ajue mzunguko wake (menstrual cycle)siku ya 1-28
2.Lazima mzunguko wako uwe na mpangilio sahihi(unaweza ukachunguza mzunguko wako kwa miezi minne mfululizo)
3.PH ya uke lazima iwe kiwango sahihi
4.Ushirikiano kati ya mwanamke na mwanaume

JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIUME
Ili uweze kupata mtoto wa kiume kisayansi unashauriwa kushiriki tendo la ndoa siku ambayo yai litakuwa limetoka kama mzunguko wako uko sahihi ni siku ya 14
Njia nyingine ya kujua yai limetoka baba anaingiza vidole viwili ukeni wakati wa asubuhi na ukikuta uteute ujue yai limetoka kwahiyo jioni mnashiriki tendo la ndoa kwa ajili ya kupata mtoto wa kiume

KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI YAI LIMETOKA ILI KUPATA MTOTO WA KIUME?
Kisayansi chromosome Y ambayo inahusika katika kutunga mimba ya mtoto wa kiume ina spidi kubwa sana ni nyepesi na haiwezi kisihi mda mrefu kwahiyo ukishiriki tendo la ndoa wakati yai limetoka maana ake unaongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume

JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIKE
Ili ufanikiwe kupata mtoto wa kike utatakiwa ushiriki tendo la ndoa siku tatu kabla ya yai kupevuka  yani hapa ni baada ya kujua mzunguko
KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA SIKU TATU KABLA
Hii ni kwasababu  chromosome X ambazo ndo zinaunda mtoto wa kike huwa zina sifa ya kuwa na maisha marefu na kutembea taratibu hivyo yai likitolewa litakuta chromosome X ziko hai

KUNA BAADHI YA WAZEE WA ZAMANI WANAAMINI HAYA KATIKA KUPATA MTOTO WA JINSIA UNAYOTAKA
KUPATA WA KIKE
Kula samaki ,mboga za majani,matunda,bidhaa za maziwa,mbegu za matikiti majia na alzeti nk
Wakati wa kufanya tendo la ndoa mwanamke akae juu nk

KUPATA WA KIUME
Kula nyama, ndizi ,Vyakula vya chumvi kama chips ila usizidishe chumvi,karanga na vyakula vingine vya potassium na sodium
Chromosomes Y zinahitaji pH ya alkane kuliko asidi ndio maana wazee waliona hili
Kuna mengi kuhusu wazee wa zamani ila nmeongelea haya ya mlo kwa maana yana mantiki kibaiolojia

TANZANIA YATINGA HATUA YA FAINALI KOMBE LA DUNIA


Timu ya Wasichana ya Tanzania inayoundwa na Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wa Kituo cha TSC Mwanza wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia la Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu baada ya kuifunga Uingereza magoli 2-1.

Mchezo huo uliyopigwa kwenye dimba la klabu ya Lokomotive mjini Moscow nchini Urusi Tanzania iliibuka na ushindi huo mnono kupitia kwa wachezaji wake, Mastura Fadhili na Mshambuliaji Asha Omari.

Kwa upande mwingine timu ya Brazili imetinga hatua ya fainali baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya  Ufilipino.

Tanzania ambayo ndiyo mabingwa watetezi baada ya kulitwaa kombe hilo mwaka 2014, itaikabili Brazil kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kupigwa kesho kutwa huku mpaka sasa ikiwa imeruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu.


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, ameibiwa gari lake na watu wanaosadikiwa majambazi, nyumbani kwake Toangoma, jijini Dar es Salaam.

Lyaviva amesema ameshangazwa na wezi hao kupata ujasiri wa kwenda kuiba nyumbani kwake bila kujali nafasi yake ya uongozi ikiwamo ya   mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya.

”Yaani hata hawajaogopa kuja kuiba nyumbani kwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na pia kulikuwa na walinzi wawili,’ alisema.

Akizungumzia tukio hilo, Lyaniva alisema wezi hao waliingia nyumbani kwake usiku wa kuamkia juzi kwa kukata uzio na walichukua gari aina ya Toyota IST lenye namba za usajili T 920 DMQ.

“Wakati wezi hao wanaingia sikuwapo, nilikuwa safari ya kikazi mkoani Dodoma lakini kulikuwa na watu nyumbani kwangu. Hata walinzi walikuwapo lakini wamesema hawajasikia,” alisema.

”Ninao walinzi wawili na wameniambia hawakusikia chochote lakini Kamanda (wa Polisi Mkoa wa Temeke) analifanyia kazi tukio hilo maana hata mimi sielewi vizuri. Ijumaa (juzi) nilipoingia nyumbani ndipo nikapatiwa hizo taarifa,” alisema.


1. Ngono haimfanyi mwanaume asikuache, hata ukukuruke vipi, jikwatue kiasi gani kama hajaona quality za kuwa mke atakuacha tu.

2. Mwanaume anaekupata kwa vile alitumia pesa zake kwako hatakaa na wewe milele. Wanaume halisi hawawezi wakatoka na wanawake feki wanaopenda pesa. Ukibahatika sana atakufanya daraja la pili yaani mchepuko!

3. Uzuri wa mwanamke unaweza ukampelekea akaolewa ila tabia yake ndio itakayoamua ni kwa muda gani atadumu katika ndoa. Uzuri huvutia wanaume, ila tabia hufanya wanaume wadumu na wewe.

4. Pesa kiukweli ina faida sana na ni muhimu kwa mtu yoyote kuwa nayo ila pesa peke yake haiwezi kuleta ukweli wa maana halisi ya furaha na maisha.

6. Kuwa mzuri bila tabia njema hakuwezi kukakupa mume bora, sana sana utapata Boyfriends na wanaume za watu.

6. Tendo la ndoa linaleta faraja ila haliwezi kuleta upendo. Sex ni zao la mapenzi, mapenzi sio zao la sex.

7. Sex inaweza kufanya mwanaume alale na wewe usiku kucha, na asubuhi akaondoka zake ila upendo hufanya mwanaume aishi na wewe daima.

8. Kuna mambo mengine pesa haiwezi nunua kama tabia na heshima, kama ulikubali kuolewa nae kisa pesa zake. Usidhani kupitia pesa zake ataweza badilika.
9. Uvaaji wako siku zote ndio utakaoamua ni nini wanaume wazungumze na wewe!

Sunday, May 13, 2018

HUJUI KWANINI MKE WAKO ANA KISIRANI? HEMBU VAA VIATU VYAKE SIKU MOJA UTAJUA NI KWANINI!


Inawezekana anafanya kazi, kutwa nzima yuko kazini, anahangaika na bosi akitoka anarudi nyumbani, anakutana na watoto ambao hata kuoga bado, hapo hajakupikia chakula kukuandalia maji ya kuoga na kukupigia nguo pasi kisha usiku unataka mechi. Kumbuka hiyo ni kila siku tangu mwanzo wa ndoa mpaka anakufa, hivi kwanini asiwe na kisirani, hembu wewe jaribu ratiba yake kwa siku moja uone kama hutachanganyikiwa.

Lakini inawezekana hata hafanyi kazi, lakini akiamka asubuhi ni mikiki mikiki ya hapo nyumbani, mbali na kazi, kuhangaika na nepi za watoto, kuhangaika na kilio cha watoto ambao hawapendi kula lakini kuna majungu ya majirani na usiku wala hapumziki, naye ni kupika, kukupasia na kukupa mechi. Kwanini asiwe na kisirani, ana raha gani ya kumfanya kucheka kama mpaka kufa anakua katika kifungo kama hicho.

Lakini wewe ratiba yako ukitoka kazini unapitia kwa marafiki, huko unatoa stress zote kabala ya kurudi nyumbani, unakutana na kila kitu kiko sawa, kimeandaliwa mpaka taulo na mafuta ya kujipaka umeandaliwa! Hivi mtu kama wewe unakua na kisirani cha nini? Sasa mwisho wa wiki badala ya kutoka na mke wako unatoka na mchepuko wako, tena unauona kama wenyewe umechangamka ukiwa nao huboreki kwakua hauna kisirani.

Unausimulia kabisa kuwa angalau ukiwa nao una amani tofauti na mkeo ambaye kila siku ni kelele. Unasahau kuwa mchepuko unakutana nao kwaajili ya starehe, kwaajili ya kuutoa out kwamba hata kama ulikua na stress lakini si unautoa out kuziondoa sasa utazionaje. Hapa ni sawa na mtu kusema si mchafu wakati mnakutania bafuni mkioga, mkeo yeye unamhukumu kusema ni mchafu wakati umemkuta shambani analima!

Mwanamke naye ni binadamu, anahitaji kupumzika na hayo maisha ya kila siku, anahitaji kubadilisha mzunguko wake wa maisha. Kutoka Kuamka-Kupika-Kufua-Kupika-Kupasi-Kitandani na angalau mara moja hata kama ni kwa mwezi ujumlishe na kutoka out. Lakini na nyie dada zangu kama mume wako hakutoi, hajali hembu chagua siku moja ya mwezi na sema leo sitapambana na Nepi nitajitoa mwenyewe, hata umuachie watoto hapo nyumbani utoke kidogo!

NAONGEA NA WEWE!! UNAECHEZEA WANAWAKE


wewe ambae miaka mitano ya uchumba
ushamfunuafunua mtoto wa watu kama sufuria la pilau msibani, unamjua mwili wake kama unavyojua mabeti ya wimbo wa Taifa,mtoto wa watu amewakataa wanaume wengi Amepoteza muda wake kwaajili yako Amekuamini wewe ametulia anajua ndoa inafuata hivi karibuni halafu wewe ghafla tu unakuja kumzingua na kutangaza ndoa na mtu mwingine, akikuuliza sababu ya kumuacha yeye unasema siwezi kuoa mwanamke hajui kukatika kitandani nataka kuoa fundi wa kumiliki kitanda, Ulimfundisha??
kwani unaoa mke wa kujenga nae Familia au unaoa mke wa kwenda kufungua bendi ya kukata viuno??
maana kama nia yako ni kupata mke anaekatika basi ungeenda kuoa wanenguaji kwenye bendi ya Akudo Impact,mnaumiza watoto wa watu kibwegebwege na sababu za kijinga,kwani utakula kiuno
All Ur Life?? Au mtajenga uchumi wa Familia kwa kukatika kitandani?? Acha kucheza na hisia za wanawake wewe nimetupa jiwe GIZANI kama LIMEKUGUSA BADILIKA ACHA IYO TABIA NAWAPENDA WANAFAMILIA WOTE!!!

SABABU TISA (9) ZINAZOPELEKEA WATU KUFA MAPEMA ZAIDI



1.Kuangalia TV/Computer zaidi ya masaa 2 au 3.
2.Kula vyakula visivyokuwa na lishe ambavyo ni sawa na makapi.
3.Kulala kidogo au kulala sana. (Kitaalamu wastani wa muda wa kulala kwa mtu mzima ni masaa 7 mpaka 9)
4.Kuwa na mawazo mengi ya kazi au kifamilia.
5.Kuwa mpweke (kukaa bila marafiki.)
6.Kuishi bila mpenzi kwa muda mrefu.
7.Kuishi bila kuwa na furaha  (Kucheka.)
8.Kukaa mahali kwa zaidi masaa 4 au 5 au zaidi ya hayo.
9.Kuishi kwa hofu.

Namba ngapi imegusa upande wako?


BABA DIAMONDI PLATNUM AGOMBANIWA NA WAREMBO KILABUNI

Warembo wawili ambao walifahamika kwa majina ya Ashura na Zubeda, wamedaiwa kuzichapa kavukavu chanzo kikitajwa kuwa ni kumgombea baba wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma.

Tukio hilo lililokusanya watu lilitokea hivi karibuni katika baa moja maarufu kwa jina la Suma iliyopo maeneo ya Magomeni-Kagera jijini Dar ambayo baba wa msanii huyo anadaiwa kuwa anakwenda mara kwa mara kupata ‘kinywaji’.

Taarifa zaidi zinaarifu kuwa, warembo hao walitangulia kufika katika baa hiyo na kupiga stori pamoja huku wakipata kilevi lakini baadaye alipotokea baba Diamond na kujumuika nao, kila mmoja alianza kujitapa kuwa ni wake. 

“Yani walianza kubishana. Ghafla wakaanza kushikana na ndipo watu walipowawahi na kuwaamua. Baba Diamond kukwepa soo akaamua kutoweka eneo hilo,” kilidai chanzo

FUNZO KWA WENYE MICHEPUKO (HAWARA)


Kabla mahusiano yao hayajakolea
jamaa akamkalisha chini huyu mdada hawala yake na kumueleza misimamo Wake.
Jamaa akamweleza
"Mpaka tumekuwa kwenye mahusiano maana yake nimekupenda si ndio hivyo mpenzi wangu :-
Nilikwambia tangu awali nina mke na watoto.
Nampenda mke wangu ndio maana nilifunga nae ndoa.....Sitamani hata siku moja aje kuumia moyo wake eti kwasababu yako.......
Sina malengo yoyote na wewe hususani yakuoana kwa ndoa maana tayari niko na ndoa.....nakuheshimu pia kwa nafasi yako lakini kuwa na nidhamu kwenye ndoa yangu
..kukupenda wewe haina maana kwamba mke wangu simpendi no,ni udhaifu wa wanaume tulionao ...Sitaki uwasiliane na mke wangu hata mara moja
Sitaki ajue nina hawara nje ya ndoa , kwasababu mke wangu anasali anamuomba Mungu Sana .
Hata mahusiano yetu najua ataonyeshwa kwenye ndoto tu siku moja ! Ni afadhari akawa ana hisia tu lakini sio ajue kwamba nipo na wewe .
Farida akajibu " ina maana huna malengo kabisa na Mimi!!!! kwahiyo una mpango wa kunichezea tu??
Jamaa akamjibu "Kwani ulitaka nini zaidi kutoka kwangu? jamaa akamuuliza.
Farida akamjibu
""Nataka unizalie watoto namimi nataka ndoa hata mke wa pili nipo tayari siwezi kukuacha wewe my dear sweet!!!
Jamaa
Haa eti nini!? kama ni hivyo tuishie hapa hapa , dini yetu hairuhusu kawatafute wakina Yusufu Salumu sihitaji stress ndio maana nimekwambia mapema misimamo yangu kama utaiweza, huiwezi tuishie hapa....
Farida akamjibu
Haya nimekuelewa ntafuata huu utaratibu kwasababu nakupenda.alijibu farida .....
poa una amani lakini?aliuliza jamaa
Yes usijari......farida alijibu
Jamaa
Naomba ninapokuwa nyumbani usinitext wala nisiione call yako ni mpaka iwe ninapokuwa kazini tu.....
Farida
sawa mpenzi wangu sasa si uweke password kama hutaki mkeo asione simu yako?
Jamaa
Hapana sitaki kuonekana kutokuaminiwa na wife...na usichati na Mimi kwa msg za kawaida au Whatsap wala messenger,tutumiane email tu.
Farida akajibu "sawa"
................................................
Uhusiano wao uliendelea lakini Farida hakuwahi kuwa na amani kwa mapenzi yenye mashart kama yale ,ilikuwa inamuuma akikumbuka maneno ya jamaa na vile anavyo mheshimu mkewe na si yeye.....alivumilia tu kwakuwa jamaa ana hela,chochote alichotaka alipewa.
Alitumia kila mbinu ili kumvutia jamaa, alijaribu kumuuliza kitu anachokipenda huyo buana ili amfanyie mfano chakula anachopenda, lakini jamaa hakuwa muwazi Sana kwake.
Farida Alitamani sana kumjua huyo mke wa jamaa lakini hakuweza
Alijaribu kutafuta hakufanikiwa,ila mara kadhaa alimskia jamaa akiongea nae kwenye simu anamuita Magdalena.....au mama Francisco.
Siku moja akiwa saluni kwake aliyofunguliwa na jamaa akiwa na msichana wake wa kazi
Akaanza kupitia Facebook akaingia kwenye profile ya jamaa aone marafiki zake ,
Akasearch jina la Magdalene akalipata , akafungua profile yake akakuta ni kweli ni mkewe jamaa, kwanza alimuweka mumewe Picha yake ya wasifu.
Akamuomba urafiki, muda huo huo magdalena akaacept......akamshukuru kwa kumkubalia urafiki magdalena akamwambia "karibu my"
Akajibu asante....
Wakachat sana siku ile.....huyu Farida akajisemesha "nimemmaliza tayari.....usiku ule hakulala usingizi akimtafakari yule mwanamke....amfanyie nini maana ndio kikwazo kikubwa chake.
Kulipokucha mchana akiwa nyumbani kwake akamtext msichana wake
" nimeongea na huyu mshamba nimemkaribisha saluni nimemwambia tunampa ofa aje,
Sasa naomba akija hapo wewe endelea kumfumua hizo nywere zake Mimi nitamnunulia soda ntamuwekea na pilipili atajuta kunifahamu"!
Dada wa kazi pilipili!!??? aliuliza huyo binti
farida
Wewe nawe baki na hilo ilo ,namaanisha sumu!alijibu
Anhaà hapo sawa,kwahiyo nisimuwahishe niende nae taratibu?
Farida
no no wewe Fanya kawaida Mimi dakika chache ntakuwa hapo...alijib
Magdalena dakika 20 akawa amefika na gari yake ..Akamjulisha Farida akampa maelekezo msichana wake akawa amemwona akampokea.....wakaanza kazi
Dakika 10 mbele Farida akawa amefika ,story zikaendelea Magdalene hamjui Farida ,Farida anamjua Magdalena.
Baada ya kumsuka nywere akiwa karibu na kumaliza Farida akamwambia ngoja nikununulie na soda japo ukanywe hata nyumbani , soda gani vile?
"Yoyote nichukulie my dear nashukuru sana" alimjibu
Farida akajifanya kama anaenda dukani lkn alikuwa kazunguka nyuma ya saluni yake akatoa chupa ya take away kwenye pochi yake, na akapita dukani akaagiza zingine mbili za kwao na binti yake.
Akampa Magdalena soda aina ya pepsi, akashukuru akawasha gari akaondoka zake ....akionyesha kufurahishwa na Huduma zao na upendo au ukarimu wao asijue mtego wa muwindaji.
Huku nyuma walianza kupongezana wakiamini zoezi lao limefanikiwa walijua kwa vyovyote vile angekunywa njiani na kufa hapo hapo
Na iwapo angekunywa tu asingefika mbali kutokana na ujazo wa pakti za sumu aliyomimina kwenye chupa......
"sikutaka kumpa mapema halafu afie hapa sitaki mizoga ya watu hapa akafie mbele huko pumbavu kabisa" alijisemesha Farida.
Kumbe Magdalena ile soda hakunywa kwenye gari.....Akawa amefika nayo mpaka nyumbani kwake .....
na kwasababu soda ilikuwa imekuwa ya akaingia nayo ndani akaiweka kwenye friji moto na zingine.
Ikawa imelala kwenye friji.
Mchana wa kesho yake jamaa akarudi nyumbani kula chakula Alipokuwa anaondoka kurudi ofisini, akamwomba mkewe ampe soda, na soda yake kubwa ni pepsi akampa ile ya kina Farida pasipo kujua .
Patamu hapo.............
Akiwa anaondoka akaona kuna email imeingia , kucheki anakutana na text ya Farida "uko wapi my?"
Natoka nyumbani naenda ofisini, OK basi nipitie saluni Nina shida kidogo..........
Anataka amuulize maendeleo ya familia yake ,ana wasiwasi je soda ilinyweka?au ile sio sumu kadanganywa?
Jamaa alipofika Farida akaingia kwenye gari akamkiss jamaa
Wakaondoka wote kuelekea ofisini kwa jamaa.
Farida akalalamika njaa ikabidi ampitishe mahali akala akamsubiri.
walipokuwa wakiondoka akiwa kwenye gari akaona soda akamwomba anywe ,jamaa bila ajizi yoyote akampa....kumbe ni ile yenye sumu pilipili!
Na kwakuwa alikuwa kakaukiwa akaanza nayo hapo hapo! Kidi kidi kidi akakata kama nusu hivi
Huku wakipiga story........
Dakika tano peke zilikuwa ni nyingi akaanza kuskia maumivu makali hamna mfano, moja kwa moja akajua ni ile soda.....ha! Akajishika tumbo akatoa macho akamuuliza "hii umeitoa wapi? jamaa akajibu" nyumbani kwenye friji langu"
Ooooooh my god mkeo ameniua jamani! Mkeo ameniua niwahishe hospital haraka plz!
Mke wangu amekuua?
kivipi hebu niambie!!!
Dah!Kweli mkeo anasali.......
Farida anaongea huku akilia kwa uchungu mkubwa akatamka neno la mwisho akasema
"Nakufa kwa upumbavu wangu mwenyewe, niwahishe hospital labda ntapona mimi!
Jamaa dakika 15 akawa amefanikiwa kufika hospital akaingia nae ,jopo la madaktari wakiwa wanamhangaikia yeye akawa amewasha gari akatoroka kukwepa kesi .......huku nyuma Farida ikawa ndio kwa heri bye bye! Amekufa
Kuchunguzwa ikaonekana amekufa kwa kula chakula au kinywaji chenye sumu.
Kumtafuta aliyemleta hospital wakashangaa hawamwoni.na bahati nzuri simu ya marehemu akawa ameondoka nayo.
Taarifa ikafika police.
Na ilipotangazwa iwapo angetokea ndugu wa marehemu ,wa kwanza akawa ni binti wa saluni.
Police ilibidi waanze nae yeye kuchunguza simu yake, Bahati nzuri au mbaya kwake, zile Meseji walizochati na dada hakuzifuta.........
binti akawa ni mtuhumiwa namba moja ilionekana kuna MTU walimpa sumu na marehemu lakini ninani? na mbona Farida ndiyo amekufa tena?wakaenda kuirenew ile line ya marehemu.
Upelelezi ulipokuwa ukiendelea tayari yule binti akabanwa mpaka akakiri kuhusu mpango waliousuka na marehemu dhidi ya mke wa jamaa aitwaye japhert..... Walipomtafuta akaja japhert pamoja na mkewe.
Magdalena akahojiwa kama anamfahamu Farida akaeleza vile walivyojuana kupitia Facebook kama wiki tatu tu.
Akaeleza vile walivyompa na ofa ya kwenda kusuka na "huyu binti ndiye aliyenisuka na wakaninunulia soda" lakini ile soda sikuinywa nikaenda nayo nyumbani.....................akasimulia kama hapo juu.
Mume akawa anashangaa anaona ni kama video move baadae mahakama ikamtia hatiani yule binti.
Walipofika nyumbani Magdalena ilibidi ambane mumewe
"Vipi Mume wangu marehemu kumbe alikuwa hawara wako?"
Ilibidi mumewe awe muwazi tu kwake,akamweleza Kisa kizima
huku akilia kwa uchungu mkubwa.......
Ni kweli Mimi ndio nilitaka kukuua kwa upumbavu wangu,naomba unisamehe,sijui kwanini wanaume haturidhiki na hatutosheki?hakuna chochote ninachokikosa kwako lakini tamaa tu!
Usimwache Mungu unayemtumikia mke wangu,ningefanyaje Mimi kukupoteza wewe!?
ningefanyaje na watoto hawa?
Mama akamfuata mkewe akamkumbatia miguu huku akilia
Jamaa akawa ameishiwa maneno ya kuongea zaidi ya "nisamehe".......wakaangua kilio cha kumshukuru Mungu.
Mwishoni mama Francisco akiwa amemkumbatia mmewe,anasema mwili wote ulikuwa kama unachemka,akasema nyamaza nimshukuru Mungu:
"EEH MWENYEZI MUNGU,BABA WA REHEMA,MUNGU UTULINDAYE,
BIBLIA IMESEMA WEWE USIPOULINDA MJI WAULINDAO WAKESHA BURE.......
USIPOILINDA NDOA, HATUWEZI KUFANYA CHOCHOTE.......
ASANTE KWA UAMINIFU WAKO KWANGU,
ULINIAHIDI IWAPO NIGEKUWA MWAMINIFU KWAKO,USINGENIACHA WALA KUNIPUNGUKIA HATA SEKUNDE TANO!
NA KWAMBA MAADUI ZANGU WANGEKUWA ADUI ZAKO. NA UMESHATIKIZA AHADI YAKO KWANGU.
ASANTE KWA KUHAKIKISHA NAZIDI KUWA SALAMA. UMETULINDA MIMI NA MUME WANGU NA WATOTO.
ILE SODA PAMOJA NA KWAMBA IMEINGIA MPAKA NDANI KWANGU, LAKINI HAKUNA ALIYEKUNYWA NAJUA NI UWEZA WAKO LAKINI HATA MMOJA WETU ANGEKUNYWA ASINGEDHURIKA MAANA UMESEMA " TUKILA VYA KUFISHA HAVITATUDHURU.........
TULINDE TUTUNZE ZAIDI KWA UTUKUFU WA JINA LAKO AMENI....